• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Kenya wawaokoa waeritrea 8 kwenye njama ya magendo ya binadamu

    (GMT+08:00) 2019-04-01 08:46:08

    Polisi wa Kenya wametangaza kuwa wamewaokoa waeritrea 8 wenye umri kati ya miaka 7 na 31, wanaoaminika kuwa ni wahanga wa biashara ya binadamu katika kaunti ya Isiolo mashariki mwa Kenya.

    Makachero kutoka kurugenzi ya upelelezi wa makosa ya jinai wameweza kuzuia gari iliyokuwa inawasafarisha watu hao kwenye njia panda ya Wamba katika kaunti ya Isiolo. Watuhumiwa watatu wamekamatwa, na mmoja alifanikiwa kutoroka kwa gari.

    Baada ya upelelezi polisi waligundua pasipoti kadhaa za wakenya, wasomali na waethiopia katika hoteli moja kwenye eneo la Eastleigh, na kusema wamiliki wa pasipoti hizo ni sehemu ya genge kubwa la wasafarishaji wa wahamiaji.

    Sakata hili limekuja siku mbili baada ya genge kama hilo kuibuliwa katika kaunti ya Kiambu, ambapo warundi 25 wenye umri kati ya miaka 24 na 33 walikuwa wakishikiliwa kusubiri kupelekwa katika nchi za Asia ikiwemo Thailand.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako