• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makumi ya watu wauawa katika mapambano kati ya vikosi vya serikali na waasi kusini mwa Yemen

    (GMT+08:00) 2019-04-01 08:53:54

    Wanajeshi wasiopungua 13 na makumi ya waasi kutoka kundi la Houthi wameuawa jana kwenye mapambano yaliyotokea mkoani Dhalea, kusini mwa Yemen.

    Mapambano hayo yalitokea baada ya waasi hao kudhibiti ngome zilizoko kaskazini mwa Dhalea siku tatu zilizopita, umbali wa kilomita 245 kutoka kusini mwa mji mkuu Sanaa. Vikosi vya serikali vimetwaa tena ngome hizo kutoka kwa waasi baada ya mapambano hayo yaliyosababisha vifo na majeruhi wengi.

    Wakati huo huo, mjumbe wa kundi la Houthi Mohammed Abdulsalam jana alikutana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Griffiths nchini Oman, ambako wamejadiliana kuhusu njia ya kumaliza mvutano kwenye mchakato wa kutimiza amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako