• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa UM kuhusu uhifadhi wa maji na ardhi wafunguliwa Cairo

    (GMT+08:00) 2019-04-01 08:54:21

    Mkutano wa Mashariki ya Karibu na Afrika Kaskazini wa kuadhimisha Siku ya Ardhi na Maji ya mwaka 2019 ulifunguliwa Jumapili mjini Cairo.

    Mkutano huo wa siku tano ulioitishwa na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa mataifa FAO umevutia wataalamu, watendaji, maofisa wa serikali, watunga sera na washirika wa maendeleo zaidi ya 400 kutoka nchi za Mashariki ya Karibu na Afrika Kaskazini NENA na sehemu nyingine duniani.

    Mkutano huo unalenga kubadilishana ujuzi na kujadili ufumbuzi wa tatizo la ukosefu wa maji na chakula, na usimamizi wa kuvia kwa udongo na ardhi kubadilika kuwa jangwa, kutokana na ukame na mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na masuala mengine yanayohusiana na maisha ya binadamu.

    Katibu mkuu msaidizi wa FAO na mwakilishi wa FAO kanda ya NENA Bw. Abdessalam Ould Ahmed, amesisitiza kuwa masuala yatakayojadiliwa katika siku zijazo ni muhimu kwa kanda hiyo, kwa kuwa yanaweza kukwamisha ukuaji wa uchumi, kuongeza umaskini na hatimaye kuharibu amani na utulivu wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako