• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wapinga uamuzi wa Trump wa kutambua mamlaka ya Israel kwa milima ya Golan

    (GMT+08:00) 2019-04-01 08:54:44

    Ofisa mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini, amesema Umoja wa Ulaya unapinga uamuzi wa rais Donald Trump wa Marekani wa kutambua mamlaka ya Israel kwenye milima ya Golan nchini Syria.

    Akiongea kwenye mkutano wa 30 wa kilele wa Jumuiya ya nchi za kiarabu uliofanyika mjini Tunis, Bibi Mogherini amesema uamuzi huo wa Marekani unakwenda kinyume na maazimio ya Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, ambayo yanaitambua milima ya Golan kuwa ni ardhi ya Syria inayokaliwa na Israel.

    Bibi Mogherini amesema Umoja wa Ulaya unajitahidi kufikia suluhu ya kisiasa ya msukosuko huo kulingana na maazimio ya Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, na kusisitiza kuwa suluhu ya kisiasa itakuwa ni njia pekee ya amani ya kukomesha mgogoro nchini Syria, na kuhakikisha masuala ya pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako