• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini kuongeza uzalishaji wa mafuta hadi mapipa elfu 70 kwa siku mwezi Juni

    (GMT+08:00) 2019-04-01 09:07:59

    Sudan Kusini inapanga kurejesha uzalishaji wa mafuta katika maeneo matatu ya mafuta yaliyofungwa, na kuongeza uzalishaji huo hadi mapipa elfu 70 kwa siku katika mwezi wa Juni.

    Wizara ya mafuta na madini imetoa taarifa ikisema maeneo ya mafuta ya El-Nar, El-toor na Manga yaliyoko kaskazini mwa nchi hiyo, yatarejesha uzalishaji Aprili 27 kwa lengo la kuongeza uzalishaji hadi mapipa elfu 70 kwa siku kabla ya mwezi wa Juni.

    Uamuzi huo umetolewa baada ya waziri wa mafuta wa Sudan Kusini Bw. Ezekiel Lol Gathuoth na mwenzake wa Sudan Bw. Ishag Adam Bashir Gamaa kutembelea maeneo hayo Jumamosi.

    Mawaziri hao pia wamesaini makubaliano ya kuruhusu makampuni ya mafuta yanayozalisha mafuta nchini Sudan Kusini kutumia ardhi ya Sudan kusafirisha vifaa vya uzalishaji wa mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako