• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha wafanywa Dar es Salaam

    (GMT+08:00) 2019-04-01 18:44:32

    Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imefanya ukaguzi katika maduka ya fedha na kusababisha mengi kufungwa . Hii inatokana na juhudi za serikali za kudhibiti ubadilishaji holela wa fedha za kigeni.

    Jiji hilo linakuwa la pili baada ya ukaguzi kama huo kufanyika Arusha mwishoni mwa mwaka jana na kushuhudia maduka kadhaa kufungwa kutokana na kukiuka sheria na mengine kutokidhi sifa zinazotakiwa.

    Oparesheni hiyo ilifanywa kwa pamoja na maofisa wa BoT, wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na maofisa wengine wa Serikali.

    Wachambuzi wa mambo ya biashara wamesema hatua hiyo huenda ikapunguza kasi ya biashara katika maeneo ya Kariakoo ambako wafanyabiashara, hasa wa nguo na vifaa vya kielektroniki hutegemea wateja kutoka nchi za jirani. Wafanyabiashara hao hutumia maduka hayo kubadilisha fedha na kuzitumia kufanya manunuzi kwa ajili ya kupeleka kwenye nchi zao, hasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Zambia na Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako