• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watalii yatarajiwa kuongezeka Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-04-01 18:45:03

    Idadi ya watalii na fursa za biashara zinatarajiwa kuongezeka nchini Rwanda na Tanzania kufuatia ushirikiano wa watoaji huduma za utalii kutoka nchi hizo mbili. Haya yametokana na mkutano wa kuzungumzia fursa za kibiashara haswa za kitalii uliowaleta pamoja watoaji huduma hizo kutoka nchi zote mbili mjini Kigali Rwanda. Wadau hao wa utalii walisema kuna haja kutilia mkazo zaidi vivutio vya pande zote mbili kama vile hifadhi za Sokwe nchini Rwanda,ziwa Kivu pamoja na msitu wa Nyugwe. Naibu mwenyekiti wa chama cha kutoa huduma za kitalii nchini Rwanda bi Carolyn Namatovu amesema ushirikiano huo unalenga kupiga jeki sekta ya utalii katika nchi zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako