• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bodi ya maziwa Tanzania kuinua wafugaji

    (GMT+08:00) 2019-04-01 18:45:24

    Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imeandaa mkakati wa kuwawezesha wafugaji kuongeza tija ya kazi zao kwa kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini,.

    Mkakati huo unahusisha kuwakopesha ng'ombe wanaotoa maziwa mengi kwa bei na masharti nafuu pamoja na kuwajengea uwezo wa kufuga kisasa.

    Kufanikisha hilo, kaimu msajili wa bodi hiyo, Dk Sophia Mlote amesema wanashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na wanaanza na Mkoa wa Tanga ambako tayari kuna mitambo 350.

    Akizungumza na wafugaji, Dk Sophia amewataka kuanzisha mashamba ya malisho kwa ajili ya mifugo waliyonayo.

    Tanzania inazalisha lita bilioni 2.4 za maziwa pekee kwa mwaka.

    Kwa uzalishaji huo, inakadiriwa kila Mtanzania anakunywa lita 47 kwa mwaka badala ya 200 zinazopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

    Miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili wafugaji ni malisho duni, magonjwa na elimu ndogo ya ufugaji na isiyozingatia kanuni bora za ufugaji hali inayoshusha uzalishaji wa maziwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako