• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapato yatokanayo na mauzo ya nje yaongezeka

    (GMT+08:00) 2019-04-01 18:45:41

    Mapato yatokanayo na mauzo ya nje nchini Rwanda mwaka jana yaliongezeka na kufikia dola milioni 995.7 kutoka dola milioni 943.5 mwaka wa 2017 ikiwa ni ongezeko la asilimia 17. Hata hivyo taarifa zinasema kuwa pengo la biashara liliongezeka kwa asilimia 12.4. Wachambuzi wanaona gharama ya uagizaji bidhaa umetokana na ujenzi wa miundo mbinu unaoendelea hivi sasa nchini humo. Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha umeme cha Peat, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Bugesera na miradi ya upanuzi wa barabara.

    Wakati huo huo sekta ya madini nchini humo imeendelea kufanya vizuri huku madini yanayosafirishwa nje zaidi yakiwa ni Coltan miongoni mwa mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako