• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yaeleza wasiwasi wake dhidi ya vurugu kwa raia wa kigeni nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2019-04-01 18:46:02

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeeleza wasiwasi wake kutokana na vurugu dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.

    Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema, mashambulizi hayo yanayowalenga raia wa kigeni, wakiwemo wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi katika eneo la Durban mkoani Kwazulu-Natal, yamesababisha vifo vya watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa.

    Makundi ya watu waliobeba fimbo za chuma na mapanga yalivamia nyumba za raia wa kigeni na kuwafukuza, huku wakiiba mali zao, pia maduka kadhaa yanayomilikiwa na wageni yalivamiwa na bidhaa kuibiwa, kuharibiwa ama kuchomwa moto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako