• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Udhibiti wa dawa za kulevya wahitaji hatua ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-04-01 20:15:43

    Kuanzia tarehe mosi Mei, China itaweka dawa zote zenye Fentanyl kwenye orodha ya dawa za kulevya zinazodhibitiwa na serikali, ikimaanisha kuwa China itadhibiti dawa za Fentanyl kwa hatua kali zaidi.

    Ikiwa nchi iliyoathiriwa na inayoathiriwa na dawa za kulevya, China siku zote inatekeleza sera kali ya kupiga marafuku dawa hizo. Hatua mpya dhidi ya dawa za Fentanyl inaonesha kuwa China inabeba majukumu yake katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya za aina zote.

    Fentanyl ni dawa za kupunguza maumivu zenye nguvu kubwa. Katika miaka ya hivi karibuni wahalifu wa nchi kadhaa zikiwemo Marekani na Canada wanatengeneza dawa hizo na kuzifanya kuwa dawa za kulevya. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Maradhi cha Marekani, mwaka 2016 watu waliofariki kutokana na kutumia dawa za kulevya za Fentanyl walifikia 18,335. Badala ya kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti dawa za kulevya, Marekani imepaka matope China kwa kusema China ni chanzo muhimu cha dawa za Fentanyl kuingizwa nchini Marekani.

    Naibu mkurugenzi wa kamati ya kupambana na dawa za kulevya ya China, Bw. Liu Yuejin amesema, polisi wa China waliwahi kugundua baadhi ya watu wanaotengeneza na kusafirisha kiharamu Fentanyl nchini Marekani, lakini sio nyingi kiasi cha kuwa chanzo muhimu. Amesema katika suala la kushughulikia Fentanyl, China imedumisha ushirikiano wa karibu na Marekani.

    Ukweli ni kwamba dawa nyingi mpya za kulevya zimevumbuliwa na maabara ya nchi za magharibi, na pia zinatengenezwa na kutumiwa haswa katika nchi hizo. Suala la Fentanyl nchini Marekani linatokana na sababu nyingi, na serikali ya nchi hiyo inapaswa kuchukua hatua zaidi katika kupunguza matumizi ya dawa hizo.

    Ofisa mwandamizi wa taasisi ya utafiti wa sera za kimataifa za dawa za kulevya ya Chuo cha Siasa na Uchumi cha London, Uingereza Bw. John Collins mwaka jana alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC alisema, licha ya kudhibiti utoaji wa nchi za nje, Marekani inapaswa kuchukua hatua zaidi ili kukabiliana na changamoto ya dawa za kulevya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako