• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa New Zealand

    (GMT+08:00) 2019-04-01 21:05:25

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa New Zealand Bi. Jacinda Ardern, ambaye yupo ziarani nchini China.

    Rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na New Zealand kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendelea kuongoza nchi nyingine za magharibi. Amesema kutokana na hali mpya duniani, nchi hizo mbili zinapaswa kuongeza maelewano na uaminifu, na kufuata mawazo ya kufungua mlango na kusikilizana. Aidha, rais Xi amesema China inakaribisha New Zealand kujiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Naye Bi. Ardern amesema New Zealand inatilia maanani uhusiano kati yake na China, na anatarajia ziara yake itaimarisha zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako