• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia kuitisha mkutano wa wadau kuhusu usimamizi wa vyombo vya habari

    (GMT+08:00) 2019-04-02 08:37:22

    Mkutano wa wadau unaolenga kujenga utaratibu wa kujisimamia wa vyombo vya habari nchini Zambia unatarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Lusaka.

    Mkutano huo unakuja kufuatia serikali ya Zambia kuonesha wasiwasi kuwa vyombo vya habari ambavyo bado havisimamiwi vizuri, husababisha utendaji mbaya wa kazi unaokiuka vigezo vya kitaaluma na kimaadili.

    Mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano ya vyombo vya habari Bw. Enock Ngoma, amesema lengo la mkutano huo utakaofanyika Mei 9 hadi 10 ni kufikia makubaliano kuhusu utaratibu wenye ufanisi wa kujisimamia wa vyombo vya habari utakaotekelezwa nchini Zambia, kupitisha kanuni za mienendo ya vyombo vya habari na kuanzisha kamati ya muda ya kuongoza utekelezaji wa utaratibu huo.

    Bw. Ngoma amesema mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe 250 kutoka mashirikisho ya vyombo vya habari, wamiliki wa vyombo vya habari na mashirika ya kijamii pamoja na wawakilishi wa serikali, ili kuhakikisha makubaliano yatakayofikiwa ni mwafaka kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako