• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini aahidi kuwashtaki washambuliaji dhidi ya wageni

    (GMT+08:00) 2019-04-02 08:37:43

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini ameahidi kuwafikisha mbele ya sheria wanaohusika na mashambulizi dhidi ya wageni nchini humo.

    Akilaani mashambulizi hayo, rais Ramaphosa ametoa wito kwa idara za utekelezaji wa sheria na raia wanaotii sheria kuwatambua washambuliaji hao na kuwafikisha mbele ya sheria, na kusisitiza kuwa uhalifu waliotenda kamwe hauwezi kuhalalishwa.

    Rais Ramaphosa ametoa kauli hizo baada ya mashambulizi mapya dhidi ya wageni kuibuka kwenye sehemu kadhaa za nchi hiyo, haswa mjini Durban na mkoani KwaZulu-Natal, ambako majambazi wenye nondo na mapanga waliingia kwa nguvu kwenye nyumba za wageni, kuwafukuza na kupora mali zao wiki iliyopita.

    Kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR, watu wasiopungua sita wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo, ambayo yanahusiana na maandamano ya kulalamika kuwa wageni wamechukua ajira za wenyeji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako