• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli akatishwa tamaa na uzembe kwenye ukusanyaji wa kodi

    (GMT+08:00) 2019-04-02 09:02:11

    Rais John Magufuli wa Tanzania amesema amesikitishwa na uzembe kwenye ukusanyaji wa kodi unaofanywa na mamlaka ya kodi Tanzania TRA.

    Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu ya Tanzania inasema Rais Magufuli haelewi ni kwanini TRA inakusanya kodi kutoka kwa watu milioni 2.7 peke yake, wakati Tanzania ina jumla ya watu milioni 55.

    Rais Magufuli amesema hayo muda mfupi baada ya kuwaapisha naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango Bw. Adolf Ndunguru, na naibu kamishna wa mkuu wa TRA Bw. Msafiri Mbibo.

    Rais Magufuli ameitaka TRA ipanue wigo wa kodi na kuongeza vyanzo vya mapato, na sio kuwakamua wachache.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako