• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO kutenga dola milioni 38 kudhibiti mlipuko wa kipindupindu Musumbiji

    (GMT+08:00) 2019-04-02 09:08:24

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema litatenga dola milioni 38 za kimarekani kwa ajili ya kudhibiti mlipuko wa kipindupindu katikati ya Musumbiji katika miezi mitatu ijayo.

    Tangazo hilo limetolewa na mkurugenzi wa WHO anayeshughulikia mambo ya Afrika Bibi Matshidiso Moeti katika kituo cha mambo ya dharura mjini Beira mkoani Sofala. Amesema WHO limeratibu operesheni za idara zote za afya katikati ya Musumbiji, na kushirikiana na serikali katika kuweka mpango mwafaka, ili kupunguza kwa kiasi kikubwa athari zinazotokana na kipindupindu.

    Wakati huo huo, kamati ya wakimbizi ya Norway imeonya kuwa kutokuwepo kwa vifaa vya kutosha vya afya katika kambi za wakimbizi za Nigeria kutasababisha mlipuko wa kipindupindu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Kamati hiyo imetoa wito wa kuchukua hatua ili kuzuia dharura hiyo ya kiafya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako