• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wahimiza juhudi za pamoja kupunguza hasara baada ya mavuno

    (GMT+08:00) 2019-04-02 09:30:48

    Umoja wa Afrika AU umezihimiza nchi na taasisi za Afrika kufanya juhudi za pamoja katika kupunguza hasara ya chakula baada ya mavuno ili kukabiliana na kukosekana kwa usalama wa chakula barani Afrika.

    Umoja huo umesema kwenye taarifa kuwa Afrika ikiwa bado ni bara lenye tatizo kubwa la usalama wa chakula duniani, moja kati ya watu wanne wa Afrika anasumbuliwa na utapiamlo. Umoja huo umetoa wito kwa nchi na taasisi mbalimbali kuboresha mpango wa uzalishaji wa chakula barani Afrika.

    Kwa mujibu wa Umoja huo, nchi nyingi zimefanya juhudi kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya chakula na lishe ya watu wanaoongezeka barani humo, ambao idadi yao inakadiriwa kufikia bilioni 2.5 kabla ya mwaka 2050. Umoja huo pia umesema hasara ya chakula imezidi thamani ya chakula kinachoagizwa kutoka nje kila mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako