• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China Xi Jinping akutana na ujumbe wa wazee

    (GMT+08:00) 2019-04-02 10:13:05

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na ujumbe wa wazee wakiongozwa na rais wa zamani wa Ireland Bibi Mary Robinson, katika Jumba la mikutano ya umma.

    Wakati wa mkutano wao rais Xi amesema dunia inakabiliwa na mabadiliko yasiyokuwa ya kawaida, wakati matarajio ya ushirikiano wa kimataifa, na ufumbuzi wa changamoto za kimataifa na baadaye ya jamii ya binadamu vinafikiriwa na watu wenye ufahamu zaidi.

    Amesisitiza kukuza ufahamu wa jumuiya ya pamoja ya ubinadamu, na kuijenga na kuitunza dunia ikiwa ni sayari yetu ya pamoja. Pia China mara zote inafuatilia njia sahihi ya haki na maslahi kwa kuweka haki kabla ya maslahi, na ilitoa msaada usio wa kibninafsi kwa nchi za Afrika wakati China ikiwa bado ni maskini. Pia amewafahamisha kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni pendekezo la kuzinufaisha nchi zote duniani..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako