• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya BRICS wafuatilia maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2019-04-02 19:16:05

    Mkutano wa nne wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya BRICS umefunguliwa jana huko Cape Town nchini Afrika Kusini ukiwa na kaulimbiu ya 'kushirikiana kuhimiza maendeleo endelevu'.

    Mkutano huo wa siku mbili unajadili masuala kuhusu kuimarisha ushirikiano wa fedha kati ya nchi za BRICS, kuhimiza ujenzi wa miundombinu kwa nchi wanachama na nchi nyingine zinazoendelea.

    Mkurugnezi wa benki hiyo Bw. K.V. Kamath amesema, benki hiyo itatilia maanani kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono juhudi husika za nchi za BRICS. Pia amesema, hivi sasa asilimia 80 ya mikopo ya benki hiyo inatumiwa katika sekta za mawasiliano, nishati safi, raslimali ya maji na kusafisha maji taka, na nyingine inatumiwa katika sekta za maendeleo ya miji na uhifadhi wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako