• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China kufanya ziara barani Ulaya na kuhudhuria mkutano wa 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-04-02 19:20:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, , waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atafanya ziara barani Ulaya kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 12 mwezi huu.

    Geng Shuang amesema, Bw. Li Keqiang atahudhuria mkutano wa 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya utakaofanyika Brussels, na kuhudhuria mkutano wa 8 wa viongozi wa China na nchi za Ulaya ya mashariki na kati nchini Croatia.

    Pia amesema, China inahimiza watu husika wa Marekani kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, kuboresha zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuhimiza amani na utulivu wa mlango wa bahari wa Taiwan.

    Kauli hiyo imekuja baada ya mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani John Bolton kuandika kwenye mtandao wa kijamii kuwa, Marekani itatimiza ahadi yake ya kulinda Taiwan kwenye "sheria ya uhusiano na Taiwan".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako