• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za China yatoa ufadhili kuboresha mafunzo ya ufundi stadi nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-04-02 19:22:19

    Kampuni za China zilizoko nchini Kenya zimezindua ufadhili kwa lengo la kuboresha mafunzo ya ufundi stadi nchini humo.

    Shirikisho la Uchumi na Biashara la Kenya na China (KCETA), taasisi inayowakilisha kampuni 97 zinazomilikiwa na Wachina nchini Kenya, limesema shilingi milioni 1.5 za Kenya zimetengwa ili kuwasaidia wanafunzi 15 katika awamu ya kwanza. Ufadhili huo umepewa jina la mwajiriwa wa kampuni ya Avic International, Jin Yetao, ambaye alifariki kwenye ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Machi 10 mwaka huu.

    Meneja mkuu wa Shirika la Reli na Barabara la China lenye tawi lake nchini Kenya Bw. Li Changgui amesema, ufadhili huo ni maalum unaowalenga wanafunzi wanaosoma kwenye vyuo vya ufundi stadi nchini Kenya.

    Mpaka sasa, vyuo vya ufundi stadi viwili nchini Kenya vimeonyesha nia ya kushiriki kwenye ufadhili huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako