• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Mapato ya mauzo ya samaki yaimarika Uganda

    (GMT+08:00) 2019-04-02 19:37:51

    Takwimu kutoka kwa benki kuu ya Uganda zinaonyesha kuwa nchi hiyo iliuza nje samaki wa dhamani ya dola milioni 171mwaka 2018 ikiwa ndio mauzo ya juu zaidi kuwahi kupatikana ndani ya miaka 20.

    Kwa kipindi kirefu sekta ya samaki nchini humo imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa samaki wa kutoka kutokana na usimamizi duni na uvuaji usioratibiwa.

    Mwaka 2018 Uganda iliuza nje tani 24,545.

    Kwa miaka 15 sekta ya samaki imekuwa ikileta pato la kitaifa la asilimia 2.6 nchini Uganda.

    Uganda huuza nje samaki aina ya Nile Perch na soko lake kubwa ni kwenye Umoja wa Ulaya, DRC na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako