• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Precision yazindua safari kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma

    (GMT+08:00) 2019-04-02 19:39:07

    Shirika la Ndege la Precision limezindua safari kutoka Dar es Salaam kwenda jijini Dodoma.

    Licha ya safari hizo, shirika hilo pia litakuwa linasafari za kutoka Dodoma kwenda Kilimanjaro.

    Akizungumzia uzinduzi wa safari hizo, kaimu mkurugenzi wa Precision Air, Patrick Mwanri amesema ni furaha kubwa kwao kuchangia juhudi za Serikali kuendeleza na kuyafungua makao makuu ya nchi kwa usafiri wa anga.

    Shirika hilo litafanya safari zake kwa siku sita kila wiki na Mwanri amefafanua kuwa ndege zitakuwa zinatoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kila Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Jumamosi huku Alhamisi na Ijumaa zikipitia Kilimanjaro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako