• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha uokoaji cha China chatoa vifaa vya misaada ya maafa kwa Msumbiji

    (GMT+08:00) 2019-04-03 09:07:25

    Kikosi cha uokoaji cha China jana kimetoa vifaa vya misaada ya maafa kwa mamlaka ya afya ya Msumbiji huko Beira, jimbo la Sofala ambalo limeathiriwa zaidi na kimbunga cha Idai. Vifaa hivyo vyenye thamani ya dola za marekani laki 7 ni pamoja na vifaa vya uokoaji, vifaa vya hospitali, dawa, vitanda na mahema.

    Mkurugenzi wa msaada wa matibabu ya wizara ya afya ya Msumbiji Bw. Ussene Issa amesema, misaada ya China itasaidia kupunguza shinikizo kwa sekta ya afya katika kushughulikia hali ya dharura ya sasa.

    Wakati huo huo, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohammed, ameitaka jumuiya ya kimataifa itoe fedha zaidi na misaada ya muda mrefu kwa waathrika wa kimbunga cha Idai nchini Malawi, Msumbiji na Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako