• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Bouteflika wa Algeria ajiuzulu

    (GMT+08:00) 2019-04-03 09:07:38

    Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ametangaza kujiuzulu urais, wiki kadhaa kabla ya muda wake kumalizika Aprili 28.

    Shirika la habari la Algeria APS limesema Baraza la katiba la nchi hiyo linatarajiwa kuitisha mkutano wa dharura kuidhinisha kujiuzulu kwake kabla ya kutangaza rasmi.

    Bw. Bouteflika alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa rais wa Algeria mwaka 1999, na kuchaguliwa tena mwaka 2014 kwa muhula wake wa nne wa kipindi cha miaka mitano.

    Wakati rais bouteflika alipotangaza uamuzi wake wa kugombea muhula wa tano wa urais mwezi Februari, maandamano makubwa yaliibuka kote nchini humo kupinga uamuzi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako