• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya yakaribisha uangalizi wa Umoja wa Afrika kwenye mkutano wa kitaifa unaofadhiliwa na UM

    (GMT+08:00) 2019-04-03 09:08:01

    Kiongozi wa baraza kuu la taifa amekaribisha uangalizi wa Umoja wa Afrika kwenye mkutano wa kitaifa wa Libya unaofadhiliwa na Umoja wa mataifa.

    Kauli hizo zimetolewa na Bw. Khalid al-Meshri kwenye mkutano wake na mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat mjini Tripoli.

    Taarifa iliyotolewa na baraza hilo inasema Baraza hilo linatoa wito kwa Umoja wa Afrika kutoa mchango chanya katika kupunguza uingiliaji hasi nchini Libya. Bw. Al-Meshri pia amesisitiza hitaji la kufanya uchaguzi wa rais na wabunge, na kura za maoni kuhusu katiba ya nchi hiyo.

    Kwa upande wake Bw. Mahamat amesisitiza umuhimu wa ufumbuzi wa kilibya wa msukosuko wake, akieleza haja ya kufanya mkutano wa maafikiano ya Libya miongoni mwa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika.

    Libya imeshuhudia kuongezeka kwa vurugu na machafuko tangu serikali ya Muammar Gaddafi ilipoangushwa mwaka 2011.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako