Kenya inapanga kuweka mfumo wa kisheria na udhibiti unaoyahamasisha mabenki kupanua mikopo kwa makampuni madogo na yenye ukubwa kati (SME).
Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika Bw. Peter Munya amesema makampuni madogo hayana sifa ya kupata mikopo ya benki kwa sababu yanaonekana kuwa na hatari kubwa ya kushindwa kulipa, hivyo katika miezi minne ijayo sheria itaanzishwa kwa mpango wa dhamana ya mikopo ambayo serikali itahakikisha mikopo inatolewa kwa mashirika hayo.
Bw. Munya amesema hayo kwenye mkutano wa 16 wa Mfuko wa Binafsi wa Equity na shirika la uwekezaji wa hatari.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |