• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Somalia yaahidi kukomboa sehemu zinazodhibitiwa na kundi la al-Shabaab

    (GMT+08:00) 2019-04-03 09:35:41

    Serikali ya Somalia imeahidi kukomboa sehemu zinazodhibitiwa na kundi la kigaidi la al-Shabaab kote nchini humo.

    Wizara ya Habari ya nchi hiyo imesema, katika operesheni zilizoanza Jumatatu wiki hii, jeshi la taifa la Somalia SNA limezikomboa sehemu nne huko Lower Shabelle, kusini mwa Somalia.

    Wizara hiyo imesema kwenye taarifa kwamba serikali ya Somalia inasisitiza ahadi yake ya kukomboa ngome za vijiji zinazodhibitiwa na magaidi.

    Kundi la al-Shabab lilifukuzwa Mogadishu, mwezi Agosti 2011, lakini bado linadhibiti sehemu kubwa za kusini na katikati mwa nchi hiyo, na kuendelea kufanya mashambulizi Mogadishu na sehemu nyingine, na kulenga maeneo ya umma na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, pamoja na vituo vya serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako