• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: AFCON U-17, Maandalizi yafikia ukingoni

    (GMT+08:00) 2019-04-03 10:06:37

    Maandalizi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayotarajiwa kuanza April 14 jijini Dar es Salaam Tanzania yamefikia ukingoni.

    Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru vimefungwa tangu wiki iliyopita kupisha marekebisho hayo, imeshuhudiwa nyasi za bandia zimeshawekwa katika uwanja wa Uhuru na Taifa, miundombinu inaendelea kufanyiwa ukarabati.

    Michuano hiyo itapigwa katika viwanja vitatu, Taifa, Uhuru na Chamazi Complex. Tanzania ambao ni wenyeji wako kundi A pamoja na Uganda, Angola na Nigeria. Kundi B lina timu za Cameroon, Guinea, Morocco na Senegal.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako