• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Marais waliotoa zawadi kubwa kwa timu zao za Taifa

    (GMT+08:00) 2019-04-03 10:07:14

    Ni kama mtoto au mfanyakazi anapofanya vizuri hupewa zawadi ikiwa ni ishara ya kuthamini ama kumpongeza kwa juhudi aliyofanya. Hili lipo pia katika michezo ikiwemo soka, hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa nchi wakitoa zawadi kwa wachezaji wa timu zao za taifa zilizofanya vizuri.

    Wenyewe wanapenda kumuita JPM, Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli, ametoa viwanja kwa kila mchezaji wa timu ya taifa (Taifa Stars) pamoja na Bondia Hassan Mwakinyo kwa kupeperusha vizuri bendera ya nchi hiyo baada ya kuwaalika Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, alikilialika Ikulu nchini Kenya kikosi cha timu ya taifa ya Raga wachezaji 7 kila upande cha Shujaa na kuwafanyia surprise kwa kuwapatia kitita cha shilingi milioni 200 kwa wachezaji 12 wa timu hiyo pamoja na kocha wao.

    Rais aliyemaliza muda wake Joseph Kabila: baada ya timu ya taifa ya DRC kutwaa ubingwa wa CHAN mwaka 2016 nchini Rwanda, Rais aliyemaliza muda wake nchini humo Joseph Kabila aliwazawadia timu hiyo kiasi cha franc milioni 400 na kuwanunulia wachezaji wote 23 pamoja na benchi la ufundi magari ya kifahari.

    Na mwisho ni Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria, baada ya timu ya taifa ya vijana ya Nigeria kuibuka mabingwa wa kombe la dunia vijana chini ya miaka 17 mwaka 2015 ikiwa ni mara ya tano mfululizo, Buhari alitumia Naira 30 milioni kuwazawadia kikosi hicho huku kila mchezaji pia akipatiwa Naira 1.2 milioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako