• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yarejea wito wake kwa makundi ya upinzani kujiunga na mchakato wa amani

    (GMT+08:00) 2019-04-03 18:59:44

    Serikali ya Sudan Kusini imetoa wito kwa makundi ya upinzani kujiunga na makubaliano ya amani wakati nchi hiyo ikijiandaa kuunda serikali mpya mwezi ujao.

    Waziri wa masuala ya Baraza la Mawaziri nchini humo Martin Elia Lomuro amesema, serikali iko tayari kushirikiana na makundi yenye silaha ambayo yamekataa kusaini makubaliano ya amani yaliyofikiwa Septemba mwaka jana katika juhudi za kumaliza mapigano yaliyodumu kwa miaka mitano.

    Mapema leo, rais Salva Kiir wa Sudan Kusini alikutana na mjumbe wa Shirika la Maendeleo la Kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki Bw. Ismail Wais kujadili utekelezaji wa makubaliano hayo ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako