• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwandair kuanza safari za kwenda Kinshasa mwezi huu

    (GMT+08:00) 2019-04-03 19:19:17

    Shirika la ndege la Rwanda, Rwandair limetangaza kuwa litaanza safari za kwenda Kinshasa mwezi huu.

    Mkurungezi mkuu wa shirika hilo Yvonne Manzi Makolo amesema safari hizo zitaanza Aprili 17 na zitafanyika mara tatu kila wiki.

    Rwandair itatumia ndege aina ya Boeing 737-800NG yenye viti 15 kwenye kitengo cha biashara na 136 kwenye kitengo cha kawaida.

    Yvonne Makolo, amesema kuanzishwa kwa safari hizo miongoni mwa mambo mengine zitasaidia kukuza biashara kati ya Kigali na Kinshasa.

    Kinshasa utakuwa mji wa 23 ambako RwandAir inahudumu barani Afrika na kote duniani inahudumu katika miji 27.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako