• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wachinjaji kuku na wauzaji wa samaki Dodoma watakiwa kuzingatia usafi

    (GMT+08:00) 2019-04-03 19:20:16

    Wachinjaji wa kuku na wauzaji wa samaki wabichi waliopo kwenye masoko ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuzingatia usafi katika maeneo yao wanayofanyia kazi, ili kujilinda na milipuko ya magonjwa ambayo yanayoweza kuleta madhara kwao pamoja na walaji.

    Ushauri huo ulitolewa na Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yunah, alipokuwa akizungumza na wachinjaji na wauzaji wa kuku wa soko la Miembeni jijini katika kampeni yake ya kukagua na kuhakikisha masoko yote yanakuwa safi kwa matumizi.

    Yuna alisema kuwa ili kuondokana na madhara kwenye maeneo hayo ya kuchinja na kuuza ni muhimu wahusika wakazingatia vigezo vya kujilinda na maambukizi yanayoweza kujitokeza kama vile magonjwa kwa kuweka mazingira katika hali ya usafi.

    Aidha, aliwataka kuhakikisha vifaa vinavyotumika kuchinjia vinakuwa katika hali ya usafi, hii ikiwa na pamoja na mavazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako