• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zapaswa kubeba majukumu yao kama nchi kubwa

    (GMT+08:00) 2019-04-04 08:40:36

    Rais Xi Jinping wa China alipokutana na ujumbe wa wazee Jumatatu hapa Beijing, amesisitiza kuwa mahusiano kati ya nchi kubwa yanahusiana na utulivu wa kimkakati duniani, kwa hivyo nchi kubwa zinapaswa kubeba majukumu yao maalumu.

    Rais Xi Jinping amesema uhusiano kati ya China na Marekani ni moja ya mahusiano muhimu zaidi kati ya pande mbili duniani. Anatumai kuwa Marekani itaenda sambamba na China, kudhibiti tofauti na kupanua ushirikiano, na kuendeleza kwa pamoja uhusiano kati ya nchi hizo kwenye msingi wa uratibu, ushirikiano na utulivu, ili kuimarisha utulivu na kupunguza sintofahamu duniani.

    Haya ni mafafanuzi mapya yaliyotolewa na rais Xi kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani katika hali mpya ya kimataifa, inayoshuhudia mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita.

    Kwenye mafafanuzi hayo, "Jukumu" ni neno lililotajwa mara nyingi zaidi. China na Marekani zikiwa ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, ambazo uchumi wao unachukua asilimia 40 ya uchumi wa dunia nzima, zina umuhimu mkubwa katika kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia, kulinda amani ya kimataifa na kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia. Kwa hivyo, uhusiano kati ya China na Marekani ni zaidi ya uhusiano kati ya pande mbili, na una ushawishi mkubwa kwa mazingira ya kimataifa.

    Hivi sasa dunia inashuhudia fursa mpya za maendeleo zinazotokana na mapinduzi mapya ya kisayansi na mageuzi ya kisekta, na pia inakabiliwa na hatari mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa sera za upande mmoja na kujilinda kibiashara, kukosekana kwa msukumo wa ukuaji wa uchumi wa dunia, na kuongezeka kwa matishio ya kiusalama yasiyo ya jadi. Katika hali hiyo, China na Marekani zikiwa ni nchi kubwa zenye ushawishi mkubwa duniani, zinatakiwa kubeba majukumu yao ya uongozi katika kukabiliana na hatari na kuvumbua fursa za maendeleo, badala ya kutafuta kujiendeleza zenyewe tu.

    Rais Xi Jinping amesisitiza mara nyingi kuwa ushirikiano ni chaguo bora zaidi kwa China na Marekani, na kudumisha maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani kunaendana na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili, ni matarajio ya jumuiya ya kimataifa, na pia ni majukumu ya nchi hizo mbili katika kukabiliana na mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye utaratibu wa kimataifa.

    China ikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, bado ina watu milioni 16.6 ambao hawajaondokana na umaskini, lakini China haiepuki kutekeleza majukumu yake ya kimataifa, na imefanya kadri iwezavyo.

    Marekani ikiwa ni nchi kubwa zaidi iliyoendelea duniani, ambayo inaongoza duniani katika nyanja za uchumi, sayansi na jeshi, inatakiwa kubeba majukumu yake ipasavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako