• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania asema hatarefusha muda wake uliowekwa na katiba

    (GMT+08:00) 2019-04-04 09:08:59

    Rais John Magufuli wa Tanzania amesisitiza msimamo wake kuwa hatarefusha kipindi chake cha urais, zaidi ya katiba inavyoruhusu.

    Akiongea kwenye mkutano wa hadhara mjini Newala, Rais Magufuli amesema msimamo wake kuwa urais ni kazi ya muda, na mara kipindi chake kitakapokwisha ataondoka madarakani. Amesema kwa sasa kazi yake ni kuwaletea maendeleo wa Tanzania, na kipindi chake kitakapokwisha ataondoka.

    Mwezi Januari mwaka 2017, Rais Magufuli alikataa mwito kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi kurefusha muda wake wa urais, zaidi ya katiba inavyoruhusu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako