Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres aliyefanya ziara nchini humo kuhusu maswala mbalimbali ya kikanda na juhudi zinazoendelea za kupambana na ugaidi. Rais Sisi na Bw. Guterres wamejadili maendeleo ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati haswa hali ya Libya, Syria na Yemen, nchi zinazokabiliwa na machafuko. Bw. Guterres ameahidi kuwa Umoja wa Mataifa unapenda kushirikiana zaidi na Misri katika kulinda amani na usalama katika eneo la Mashariki ya Kati. Bw. Guterres anatarajiwa kwenda Libya baada ya ziara yake mjini Cairo kabla ya mkutano wa kitaifa unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa, unaolenga kuandaa mazingira kwa ajili ya uchaguzi, ili kusaidia kumaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi nchini Libya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |