• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yaanzisha ushirikiano na UNDP ili kuhimiza haki za binadamu na amani

    (GMT+08:00) 2019-04-04 09:43:01

    Sudan Kusini imeanzisha uhusiano wa kiwenzi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP ili kuingiza uzoefu bora wa kimataifa ambayo itakuza utawala wa sheria, haki za binadamu na amani.

    Waziri wa serikali za mitaa wa Sudan Kusini anayeshughulikia mambo ya utekelezaji wa sheria na mambo ya bunge Bw. Alfred Kiri Yokwe, amesema kufuata utawala wa sheria, haki za binadamu, kuzingatia maswala ya kijinsia ni muhimu katika kurejesha amani nchini humo.

    Bw. Yokwe amesema mahakama zinatakiwa kuboreshwa ili kutekeleza sheria kwa ufanisi, kwani Sudan Kusini ina makabila mengi ambayo yanahitaji ulinzi sawa wa kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako