• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Aussems na Bocco watwaa tuzo ya mwezi Machi

  (GMT+08:00) 2019-04-04 10:49:58

  Kocha wa timu Simba ya Dar es Salaam Patrick Aussems sambamba na mshambuliaji ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo John Bocco wametwaa tuzo ya mwezi Machi inayotolewa na shirikisho la soka Tanzania (TFF).

  Aussems amechaguliwa kocha bora wa mwezi akiwashinda kocha mkuu wa Azam FC, Abdul Mingange na kocha mkuu wa Mtibwa Sukari Zuberi Katwila.

  Bocco yeye amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi kwa kuwashinda Donald Ngoma wa Azam na Jaffary Kibaya wa Mtibwa. Aussems ameifanya Simba iendelee kung'ara katika ligi hiyo ambapo kwa mwezi Machi ilishinda michezo yote mitatu iliyocheza ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo huo wa ligi kuu ya Tanzania Bara. Kwa upande wa Bocco yeye alicheza mechi zote tatu, na kutoa mchango mkubwa kwa timu yake akifunga mabao manne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako