• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Robo fainali ya Klabu bingwa Afrika-TP Mazembe yawasili jijini Dar

    (GMT+08:00) 2019-04-04 10:50:44

    Kikosi cha timu ya TP Mazembe toka DRC kimewasili nchini Tanzania jana jioni kikitokea mjini Lubumbashi DRC na kuweka kambi yake katika hoteli ya Serena tayari kuwakabili wanyama, Simba sports club ya Tanzania.

    Baada ya msafara wa wachezaji na benchi la ufundi na viongozi kutokea uwanja wa ndege, moja kwa moja ulielekea hotelini kwa mapumziko.

    Kabla ya kutua Dar wakiwa kwa ndege yao binafsi ilitua uwanja wa Songwe, Mbeya kwa ajili ya kuongeza mafuta na kufanyiwa maboresho kidogo na kupigwa upepo.

    Simba itaikaribisha Mazembe uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam jumamosi hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako