• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha uokoaji cha China chamaliza kazi nchini Msumbiji

    (GMT+08:00) 2019-04-04 18:36:15

    Kikosi cha uokoaji cha China kimefunga safari ya kurudi nchini China baada ya kumaliza kazi ya uokoaji nchini Msumbuji kufuatia nchi hiyo kukumbwa na kimbunga Idai.

    Licha ya kazi ya uokoaji, kikosi hicho kilitoa huduma za matibabu na kuua wadudu na vijidudu pamoja na misaada ya dawa, chakula na maji safi ya kunywa kwa watu walioathiriwa na kimbunga Idai.

    Kabla ya kuondoka nchini Msumbuji, waokoaji wa China walitoa msaada wa vifaa vya matibabu na uokoaji kwa wizara ya afya ya Msumbiji, na idara husika za mji wa Beira.

    Ofisa mwandamizi wa kazi ya uokoaji mjini Beira Bw. Usscne Isse ameishukuru serikali ya China kwa kupeleka timu ya uokoaji nchini humo baada ya kutokea kwa maafa ya kimbunga Idai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako