• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuandaa mkutano wa kibiashara nchini China ili kuvutia wawekezaji

    (GMT+08:00) 2019-04-04 19:11:31

    Kenya inapanga kuandaa mkutano wa kibiashara nchini China mwezi huu ili kuvutia wawekezaji nchini humo.

    Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya Bw. Moses Ikiara amesema, mkutano huo utafanyika kando ya mkutano wa pili wa Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na utawawezesha maofisa wa serikali ya Kenya na kutoka sekta binafsi kukutana na Wachina wanaotaka kuwekeza nchini Kenya.

    Pia amesema, Kenya itatumia mkutano huo kuonyesha fursa kadhaa za uwekezaji zilizoko nchini Kenya, na kuongeza kuwa Kenya ina sekta nyingi za kuwekeza ikiwemo utengenezaji, nishati, afya na kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako