• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:TADB yaunga mkono ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyama Ruvu

    (GMT+08:00) 2019-04-04 19:49:38

    Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), imeahidi kuunga mkono kwa dhati wawekezaji na wadau wengine stahiki ili kiwanda cha kusindika nyama kinachotarajiwa kujengwa Ruvu, Mkoa wa Pwani kifanikiwe na kutoa mchango mkubwa katika sekta za ufugaji na viwanda.

    Akizunguza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji siani makubaliano ya ujenzi wa kiwanda hicho kati ya Serikali na Kampuni ya NECAI ya Misri jijini Dodoma jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine, alipongeza makubaliano hayo na kusema ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa ni kati ya chachu ambazo zimekuwa zikisubiriwa katika kuongeza minyororo ya thamani katika sekta ya ufugaji na kuinua maisha ya wafugaji makini wa Tanzania.

    Alisema usindikaji nyama ni mingoni mwa minyororo ya thamani inayoupa maana ufugaji wa Tanzania na kuinua maisha ya mfugaji.

    Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ufugaji na Uvuvi, Prof. Elisante ole Gabriel, alieleza kuwa kuwapo kwa kiwanda hicho kutaibua mnyororo wa thamani utakaogusa maeneo matatu; wanyama walio hai, uzalishaji na uchakataji nyama na uongezaji wa thamani ya ngozi.

    Uanzishaji wa kiwanda hicho utakuwa ni moja ya hatua muhimu katika kuinua pato la wafugaji na kuyafanya mazao ya sekta ya ufugaji kuwa ni malighafi ya moja kwa moja kwa viwanda nchini.

    Serikali ya Rais John Magufuli inatekeleza kwa juhudi kubwa sera ya kuifanya Tanzania iwe na uchumi wa kati na wa viwanda ifikapo 2025.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako