• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafanikio ya mchakato wa maridhiano Rwanda yapongezwa kwenye mkutano kuhusu mauaji ya kimbari

    (GMT+08:00) 2019-04-05 08:27:25

    Serikali ya Rwanda imepongezwa kwa juhudi ilizofanya katika kuleta maridhiano kati ya raia wake, wakati inajiandaa kwa kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994.

    Kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa siku mbili unaofanyika mjini Kigali na kuhudhuriwa na watu 500 wakiwemo wasomi na watunga sera, aliyekuwa Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo, amesema wanasikitishwa na kilichotokea miaka 25 iliyopita, lakini wanaona fahari na kilichofikiwa sasa.

    Hata hivyo licha ya mafanikio hayo, wakuu wa kamati za kupambana na itikadi za mauaji ya kimbari na kuleta maridhiano, wanasema bado kuna changamoto ya kuenea kwa itikadi za mauaji ya kimbari kwenye mitandao ya kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako