• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yahimizwa kuuza nje bidhaa anuwai ili kupunguza urari mbaya wa biashara

    (GMT+08:00) 2019-04-05 08:42:50

    Wataalamu wa Kenya wameihimiza serikali ya nchi hiyo kuongeza uanuai wa bidhaa zinazouzwa nje ili kusaidia kupunguza urari mbaya wa biashara, ambao wamesema umeongezeka kwa asilimia 1.2 mwaka huu.

    Wataalamu hao kutoka Taasisi ya Mambo ya Kiuchumi IEA na Shirikisho la Watengenezaji Bidhaa la Kenya KAM, wamesema serikali inapaswa kuimarisha uwezo wake wa kupanua vyanzo vya mapato kupitia kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali.

    Maneja wa utafiti na sera ya kifedha wa KAM Bw. Simon Githuku amesema ukuaji wa uchumi wa Kenya umeathiriwa na muundo wa sasa wa mauzo ya nje, unaotegemea bidhaa chache na masoko machache, na Kenya inahitaji muundo mpya wa mauzo ya nje ili kupunguza urari mbaya wa biashara.

    Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya dunia, mwaka jana urari mbaya wa biashara wa Kenya ulifikia dola bilioni 10.15 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako