• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Shabiki wa Simba SC atembea kwa miguu kutoka Mbeya hadi DSM kuisapoti timu yake dhidi ya Mazembe akaribia kuwasili jijini humo.

    (GMT+08:00) 2019-04-05 09:32:52

    Unaweza ukapigwa na butwaa na kujiuliza huu ni ushabiki wa aina gani, lakini ndivyo ilivyo, shabiki wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba anayeishi mjini Mbeya Shaban Ramadhan aliyeamua kutembea kwa miguu kutoka Mbeya hadi Dar es Salaam kwa miguu kwa ajili ya kuisapoti klabu yake itakapokwaana na TP Mazembe ya DRC katika mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa Afrika, jana aliwasili Kibaha, kilomita chache kutoka jijini Dar es Salaam.

    Shabiki huyo amekuwa gumzo mitandaoni kutokana na uamuzi wake huo wa kutumia wiki nzima kuanzia Machi 26 alipotoka Mbeya, anatarajiwa kuwasili jijini Dar leo na kesho kushuhudia mtanange huo utakaopigwa uwanja wa Taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako