• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara- Tambwe akosa Penalti, Yanga yatoka sare na Ndanda

    (GMT+08:00) 2019-04-05 09:33:39

    Matumaini ya ubingwa wa Tanzania bara yamezidi kufifia, Yanga SC baada ya kulazimisha sare ya kufungana 1-1 na wenyeji Ndanda FC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara jioni ya jana uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

    Sare hiyo imeiongezea pointi moja Yanga SC na kufikisha 68 baada ya kucheza mechi 29, sasa wakiizidi kwa pointi sita tu Azam FC wanaofuatia katika nafasi ya pili, lakini furaha zaidi ni kwa mabingwa watetezi, Simba walio nafasi ya tatu na pointi zao 57 za mechi 22 tu kwani upinzani unazidi kupungua kwenye mbio za taji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako