• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wafanyabiashara wafurahia baada ya mahakama kuu kufuta agizo la NEMA la kupiga marufuku mifuko

    (GMT+08:00) 2019-04-05 19:06:30

    Wafanyabiashara wauzaji na watengenezaji wa mifuko iliyoshonwa wamepata afueni baada ya mahakama kuu nchini Kenya kufutilia mbali agizo la Mamalaka ya Mazingira nchini (NEMA) la kuipiga marufuku.

    Jaji James Makau alisimamisha marufuku ya Nema kwa wanaotumia mifuko hii akisema haikushirikisha wadau kabla ya kupinga matumizi yake.

    Jaji Makau aliamuru kesi iliyowasilishwa na wafanyabiashara wanaoiagiza mifuko hiyo kutoka ng'ambo isikizwe Mei 3, 2019.

    Aidha mahakama ilizuia Nema kuwatisha watumiaji wa mifuko hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako