• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hospitali ya Rufaa ya Mbeya yaanzisha kiwanda cha kutengeza dripu

    (GMT+08:00) 2019-04-05 19:06:50

    Katika hatua za kutekeleza maelekezo ya Rais John Magufuli ya serikali ya viwanda,hospitali ya Rufaa ya Mbeya imeanzisha kiwanda cha kuzalisha maji tiba "Dripu" za IV.

    Dripu hizo zenye ujazo wa milimita 250 na 500 zimeanza kutumika kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji hali inayosababisha kuondokana na adha ya kununua au kuagiza dripu nje ya nchi.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Dk. Godlove Mbwanji alitoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania kwa kuwaunga mkono na kuwasaidia.

    Aidha alisema kuna mpango wa kuhakikisha wanazalisha maji tiba kwa kiwango kikubwa ili kutoa huduma hiyo kwa wengine ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.

    Amesema uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza Maji Tiba hayo umetekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani na katika hatua inayofuata imeanza maandalizi ya mpango wa kutengeneza dawa ya macho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako