• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Deni la umma nchini Uganda limeongezeka hadi Shs44.67 trilioni.

    (GMT+08:00) 2019-04-05 19:07:14

    Haya ni kwa mujibu wa Ripoti ya Wizara ya Fedha nchini humo.

    Ongezeko hilo linawakilisha asilimia 22 ya ongezeko katika mwaka wa fedha ulioisha Juni 2017/2018 kutoka Shs36.7 trilion katika mwaka wa fedha 2016/17.

    Kulingana na takwimu katika Ripoti za Wizara ya Fedha na taarifa za kifedha,ongezeko hilo limesababisha nakisi katika ufadhili kutoka dhamana zenye thamani ya Shs1.7 zilizolengwa kutumika katika miradi ya miundombinu kama vile barabara na nishati.

    Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa uzalishaji nishati ya maji wa Karuma na uwanja wa ndege wa Kabale.

    Hata hivyo Ripoti hiyo inasema kuwa licha ya ongezeko hilo,deni hilo linaweza kushughulikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako