• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru ya tisa ya mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yamalizika

    (GMT+08:00) 2019-04-07 17:26:25

    Duru ya tisa ya mazungumzo ya kibiashara ya ngazi ya juu kati ya China na Marekani ilifanyika tarehe 3 hadi 5 mwezi huu mjini Washington. Mazungumzo hayo yaliendeshwa kwa pamoja na naibu waziri mkuu wa China Bw Liu He ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa China kwenye mazungumzo, na mjumbe wa mambo ya kibiashara wa Marekani Bw Robert Lighthizer na waziri wa fedha wa Marekani Bw Steven Mnuchin.

    Pande mbili zilijadiliana juu ya mswada wa makubaliano mbalimbali yakiwemo kuhamisha teknolojia, ulinzi wa haki miliki ya ubunifu, hatua zisizo ushuru wa forodha, sekta za huduma na kilimo, uwiano wa biashara, mfumo wa utekelezaji na mengineyo, na mazungumzo hayo yalipata maendeleo. China na Marekani ziliamua kujadiliana zaidi kwa njia zenye ufanisi ili kutatua masuala yaliyobaki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako